Welcome to UMK Global — Ufalme wa Mungu Kwanza

TUSICHANGANYE UFALME WA MUNGU NA DINI.
Featured Articles

TUSICHANGANYE UFALME WA MUNGU NA DINI.

UMK GlobalSeptember 27, 2026UMK Insight

MATHAYO 6:33

Bali utafuteni kwanza UFALME WAKE, na HAKI YAKE; na hayo yote mtazidishiwa.

DINI NI NINI?

Dini ni Neno lenye asili ya Kiarabu, “Diin” maana yake ni NJIA.

Dini ni Njia na mfumo wa Imani wa kumtafuta na kumwabudu Mungu au miungu.

DINI NI NJIA

Mwanadamu alipomwasi Mungu kwenye Bustani ya Eden alipoteza Njia na Mfumo sahihi wa Imani wa kumwabudu Mungu (Alipoteza Mfumo wa Ibada ya Ki Mungu).

MWANZO 3:24

Basi AKAMFUKUZA HUYO MTU, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, KUILINDA NJIA YA MTI WA UZIMA.

Kwa kuwa Mungu alipomuumba Mwanadamu alimwekea mbegu ya Ibada ndani Yake, Mwanadamu alianza kutafuta Njia hizo za kumwabudu Mungu ndo akaangukia kwenye kitu tunachokiita DINI.

KUMBUKA HILI USIJE UKASAHAU; MWANADAMU YEYOTE ASIPOONYESHWA NJIA SAHIHI YA KUMWABUDU MUNGU NA MUNGU SAHIHI ANAYEPASWA KUABUDIWA ANAWEZA KUABUDU CHOCHOTE HATA JIWE AU MTI KWA SABABU KILA MWANADAMU AMEUMBIWA IBADA NDANI YAKE.

YOHANA 4:21-24

Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

NINYI MNAABUDU MSICHOKIJUA; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo WAABUDUO HALISI watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

DINI SIYO HATIMA BALI NI NJIA INAYOKUPELEKA KWENYE AMA UFALME WA MUNGU AU UFALME WA SHETANI.

MITHALI 16:25

Iko NJIA (DINi) ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni NJIA (DINI) ZA MAUTI.

YEREMIA 6:16

BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.

YOHANA 14:6

Yesu akamwambia, MIMI NDIMI NJIA, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

ANAYEMBADILISHA MTU WA DINI NA KUMUINGIZA KWENYE UFALME WA MUNGU NI ROHO MTAKATIFU.

KAMA UPO KWENYE DINI YA WAKRISTO NA HUNA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU WEWE NI FARISAYO NA SADUKAYO.

MATHAYO 11:12

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

MATENDO YA MITUME 1:8

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

ANAYETOFAUTISHA KATI YA DINI NA UFALME WA MUNGU NI ROHO MTAKATIFU

Wengi wameishia kwenye Dini Kwa wakifikiri Dini ni Ufalme wa Mungu

Mathayo 7:13-14

Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na NJIA NI PANA IENDAYO UPOTEVUNI, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na NJIA IMESONGA IENDAYO UZIMANI, nao waionao ni wachache.

Yesu hakuja duniani kuleta Dini ya WAKRISTO Bali alileta UFALME WA MUNGU. LUKA 4:43

Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya UFALME WA MUNGU katika miji mingine pia; maana KWA SABABU HIYO NALITUMWA.

URITHI WETU SIYO DINI YA WAKRISTO BALI NI UFALME WA MUNGU. MATHAYO 25:34

Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

Wengi katika harakati za kumtafuta Mungu tumeishia kwenye Dini (njia),

TUMEISHIA NJIANI.

YESU KRISTO NDIYE NJIA (Mfumo sahihi wa kumwabudu Mungu) KWELI (Neno la Mungu) NA UZIMA (Ufalme wa Mungu) YOHANA 14:6

NITAELEZA ZAIDI KWENYE VIDEO ZINAZOKUJA. USIACHE KUFATILIA.

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

© MCHUNGAJI NA MWALIMU

© Dawson. R. Kabyemela

© Ufalme wa Mungu Kwanza (UMK)

© Kingdom Influence Network

© All Around Rest (AAR)

© umkglobal.org

© www.aar.co.tz

© 0714 606 500

© 2 Nyakati 15:15

© Mathayo 6:33

© Isaya 42:6-7

© U M K

© A A R

Community Discussion

Comments(0)

Share your thoughts and join the conversation.

0/2000
Loading comments...
U

UMK Global

UMK Global publishes Kingdom-centered content that equips individuals, families, businesses and organizations through Biblical wisdom, education, technology and leadership.

Continue Reading

Related Articles

Discover more Kingdom-centered insights from UMK Global.

UKITAKA KUJUA SURA YAKO HALISI JITAZAME KWENYE KIOO AMBACHO NI NENO LA MUNGU
Featured Articles

UKITAKA KUJUA SURA YAKO HALISI JITAZAME KWENYE KIOO AMBACHO NI NENO LA MUNGU

September 27, 2026

WENGI TULIDANGANYWA KUHUSU UHALISIA WA SURA ZETU. ANZA KUJITAZAMA KWENYE KIOO HALISI(Neno la Mungu) ILI UWE NA MTAZAMO SAHIHI KUHUSU MAISHA YAKO.

TUNATUMIA NGUVU NA JUHUDI NYINGI SANA KUTAFUTA PESA NA PESA TUNAPOIPATA HATUNA TABIA YA KUTAFAKARI TULICHOKIPOTEZA WAKATI TUKIITAFUTA PESA.
Featured Articles

TUNATUMIA NGUVU NA JUHUDI NYINGI SANA KUTAFUTA PESA NA PESA TUNAPOIPATA HATUNA TABIA YA KUTAFAKARI TULICHOKIPOTEZA WAKATI TUKIITAFUTA PESA.

September 27, 2026

<p>KINACHOPOTEA WAKATI TUNAITAFUTA PESA KINA GHARAMA KUBWA SANA ZAIDI YA PESA TUNAYOIPATA.</p>

UKIONA WATU WANAKUFUATA HAWANA HAJA NA WEWE BALI WANA HAJA NA MATUNDA YAKO / KIPAWA CHAKO
Featured Articles

UKIONA WATU WANAKUFUATA HAWANA HAJA NA WEWE BALI WANA HAJA NA MATUNDA YAKO / KIPAWA CHAKO

September 27, 2026

<p>HATUENDI KWENYE MWEMBE KWA AJILI YA MWEMBE BALI KWA AJILI YA MAEMBE</p> <p>KAMA MWEMBE HAUNA MAEMBE HAUNA MAANA HAKUNA MWENYE HAJA NAO.</p>