Welcome to UMK Global — Ufalme wa Mungu Kwanza

NENO LA MWANZILISHI

Ufalme wa Mungu Kwanza. Mafanikio yatafuata.
Mathayo 6:33.

Hii ndiyo kauli mbiu yetu, Ufalme wa Mungu Kwanza, Mafanikio yatafuata, Mathayo 6:33. Tunaamini kwamba Injili ya Ufalme wa Mungu ni mfumo wa maisha unaoweza kubadilisha familia, jamii, biashara na mataifa. Kupitia bidhaa, elimu na teknolojia, tunakusudia kupeleka ujumbe wa Ufalme wa Mungu kwa watu wa mataifa yote. Karibu tuwe sehemu ya safari hii ya kuleta mabadiliko ya kiroho, kijamii na kiuchumi duniani.

UMK Global About
KUHUSU UMK GLOBAL

Maono Yanayochochea Mabadiliko

UMK Global Story

Badilisha Maisha yako Kupitia kanuni za Ufalme wa Mungu

Ufalme wa Mungu Kwanza (UMK) Global ni taasisi inayounganisha Injili, Biashara, Elimu na Teknolojia ili kueneza ujumbe wa Ufalme wa Mungu kitaifa na kimataifa. UMK Global imejengwa juu ya msingi wa Mathayo 6:33: "Bali utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."

Lengo letu ni kujenga mfumo endelevu unaogusa maisha ya watu kupitia mafundisho, bidhaa, huduma na majukwaa ya kidigitali.

Vitengo vyetu

Kusudi Letu

Maono & Dhamira

Kila tunachofanya kinaongozwa na maono yaliyo wazi na dhamira yenye kusudi, inayolenga kubadilisha maisha ya watu kupitia kanuni za Ufalme wa Mungu.

Maono yetu (Our Vision)

Kuwa madhabahu ya kimataifa ya kutangaza, kufundisha na kueneza Ufalme wa Mungu kupitia bidhaa, elimu na teknolojia na kuhakikisha kila mtu uzao wa mwanamke anapata nafasi ya kuisikia Injili ya Ufalme wa Mungu na kuingia.

Dhamira yetu (Our Mission)

Kuhubiri Injili ya Ufalme wa Mungu kwa ufunuo, kuwafungua waliopofushwa kiroho, kuwatoa waliotekwa na kuwaongoza watu wote kuingia katika Ufalme wa Mungu kupitia bidhaa, huduma na teknolojia.

Thamani yetu

Kanuni zinazoongoza kila tunachokifanya

Maadili yetu yanafafanua utamaduni wetu, yanaongoza maamuzi yetu, na yanatuhamasisha katika namna tunavyowahudumia watu binafsi, mashirika na jamii.

Mungu Kwanza

Tunamtanguliza Mungu katika kila uamuzi, kila mradi na kila mahusiano.

Ukweli wa Kibiblia

Neno la Mungu ndilo msingi wetu wa uongozi, kujifunza na mabadiliko ya maisha.

Ubora

Tunajitahidi kufikia viwango vya juu zaidi katika huduma, ubora na uboreshaji endelevu.

Uadilifu

Tunatenda kwa uaminifu, uwajibikaji na uwazi katika kila jambo tunalofanya.

Ubunifu

Tunathamini ubunifu na teknolojia ili kutatua changamoto halisi za maisha kwa ufanisi.

Huduma

Tupo kwa ajili ya kuwahudumia watu kwa unyenyekevu, huruma na kuleta matokeo yenye kudumu.

Our Impact

Kukua Hatua kwa Hatua

Kila hatua tunayofikia inawakilisha watu tuliowafikia, maisha tuliyoyagusa na msingi tunaoujenga kwa ajili ya kuleta athari kubwa zaidi katika miaka ijayo.

500+

Vitabu Vilivyosambazwa

Machapisho yanayozingatia Ufalme wa Mungu, yaliyosambazwa kwa wasomaji ili kuimarisha uelewa wao wa Biblia na Neno la Mungu.

166+

Jumuiya Inayokua

Watu wanaounganishwa kupitia majukwaa yetu ya kujifunza na jumuiya, huku idadi yao ikiongezeka kila mwezi.

10+

Bidhaa zenye Chapa ya UMK

Bidhaa za UMK Global zilizoanzishwa ili kueneza dhamira yetu na kueneza Ufalme wa Mungu.

∞

Maono ya Baadaye

Tunajenga jukwaa la muda mrefu litakaloendelea kuwahudumia vizazi vijavyo kupitia elimu, teknolojia na maadili ya Ufalme wa Mungu.

Join Our Journey

Be Part of the Vision

UMK Global is building a Kingdom-centered movement through education, technology, entrepreneurship and Biblical values. We invite you to learn, grow and make an impact together with us.