Welcome to UMK Global — Ufalme wa Mungu Kwanza

UFALME WA MUNGU NI NINI!!??
Elimu ya Ufalme

UFALME WA MUNGU NI NINI!!??

UMK GlobalSeptember 27, 2026UMK Insight

MATHAYO 6:33
Bali utafuteni kwanza UFALME WAKE, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Ufalme wa Mungu ni Mfumo wa utawala uliobeba uwepo wa Mungu Kwa misingi ya Haki, Furaha na Amani katika Roho Mtakatifu.

Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. WARUMI 14:17

Ufalme wa Mungu ni Mazingira yenye na yaliyobeba Uwepo wa Mungu (Bustani ya Edeni)

BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
MWANZO 2:15

Ufalme wa Mungu ni ushawishi wa Mungu unaotawala juu ya eneo lake, akiweka mapenzi yake, kusudi lake na nia yake, kuzalisha raia na watu wanaoelezea utamaduni wake na kuakisi asili yake.

Ufalme huathiriwa na akili ya mfalme sio sheria ya kundi la watu, ndio maana Yesu alisema ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe duniani kama huko mbinguni. MATHAYO 6:9-10

Ufalme wa Mungu ni Roho Mtakatifu ndani yetu.

wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu. LUKA 17:21

Ndugu usiache kuomba Ufalme wa Mungu uje katika Kila eneo la maisha yako maana huo ndiyo Mfumo wa mafanikio yetu.

Kama vile samaki ambavyo hawezi kufanikiwa nje ya maji vile vile na Wewe huwezi kufanikiwa nje ya Ufalme wa Mungu.

NITAELEZA ZAIDI KWENYE VIDEO ZINAZOKUJA. USIACHE KUFUATILIA.

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

© MCHUNGAJI NA MWALIMU
© Dawson. R. Kabyemela
© Ufalme wa Mungu Kwanza (UMK)
© Kingdom Influence Network
© All Around Rest (AAR)
© www.aar.co.tz/umk
© www.aar.co.tz
© 0714 606 500
© 2 Nyakati 15:15
© Mathayo 6:33
© Isaya 42:6-7
© U M K
© A A R

Community Discussion

Comments(0)

Share your thoughts and join the conversation.

0/2000
Loading comments...
U

UMK Global

UMK Global publishes Kingdom-centered content that equips individuals, families, businesses and organizations through Biblical wisdom, education, technology and leadership.

Continue Reading

Related Articles

Discover more Kingdom-centered insights from UMK Global.

ENDELEA NA MAMBO YAKO LAKINI KUMBUKA USALAMA WAKO NI KUWA NDANI YA SAFINA (Ufalme wa Mungu) MUDA WOTE ILI GHARIKA LIKIJA UWE SALAMA.
Elimu ya Ufalme

ENDELEA NA MAMBO YAKO LAKINI KUMBUKA USALAMA WAKO NI KUWA NDANI YA SAFINA (Ufalme wa Mungu) MUDA WOTE ILI GHARIKA LIKIJA UWE SALAMA.

September 27, 2026

<p>SAFINA YETU NI UFALME WA MUNGU INGIA ILI UWE SALAMA.</p> <p>KUMBUKA NJIA NA MLANGO PEKEE WA KUINGIA KWENYE SAFINA (Ufalme wa Mungu) NI YESU KRISTO.</p>

NDUGU MPENDWA, ENDELEA NA MAMBO YAKO LAKINI HAKIKISHA TAA YAKO INA MAFUTA YA KUTOSHA ILI YESU ATAKAPORUDI USIACHWE.
Elimu ya Ufalme

NDUGU MPENDWA, ENDELEA NA MAMBO YAKO LAKINI HAKIKISHA TAA YAKO INA MAFUTA YA KUTOSHA ILI YESU ATAKAPORUDI USIACHWE.

September 27, 2026

<p>NAKUOMBEA NEEMA YA MUNGU IKUSAIDIE UWE NA BUSARA YA KUHAKIKISHA TAA YAKO INA MAFUTA YA KUTOSHA MDA WOTE ILI ATAKAPORUDI BWANA YESU USIACHWE.</p>

NINI MAANA YA KUTAFUTAUFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE.
Elimu ya Ufalme

NINI MAANA YA KUTAFUTAUFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE.

September 27, 2026

<p>Adam wa Kwanza alipoteza Ufalme wa Mungu kwenye Bustani ya Edeni na Adam wa pili (Yesu Kristo) alikuja kurudisha Ufalme wa Mungu uliopotezwa na Adam kwenye Bustani ya Edeni.</p>