U
UMK Admin
Topic author
Migogoro inaweza kutokea katika mahusiano, ndoa na familia. Muhimu si kukosekana kwa migogoro, bali namna inavyoshughulikiwa. Topic hii itajadili mbinu za kutatua migogoro kwa mazungumzo, kusikilizana, kusameheana, kuweka mipaka na kutafuta suluhisho linaloheshimu pande zote.
Maswali ya kuchochea mjadala:
Tunapaswa kufanya nini tunapokuwa na hasira na mwenza?
Kuna tofauti gani kati ya kutatua tatizo na kumshinda mwenzako?
Ni wakati gani ni muhimu kuhusisha mshauri au mtu wa tatu katika kutatua mgogoro?
